Jumatano, Januari 27, 2016

MASANAMU UCHI YAFUNIKWA ROMA, KWA HESHIMA YA RAIS ROUHANI

Masanamu yote uchi ya Jumba la Makumbusho la Capitoline katika mji mkuu wa Italia, Roma yamefunikwa wakati wa mkutano wa Rais Hassan Rouhani na Waziri Mkii wa Italia, Matteo Renzi.
Msemaji wa jiji la Roma amesema uamuzi wa kufunikwa masanamu yote uchi ya Jumba la Makumbusho la Capitoline kwa heshima ya Rais Rouhani ulichukuliwa na ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Shirika la habari la Italia, ANSA limeripoti kuwa masanamu ya jumba hilo la makumbusho yamefunikwa kwa heshima ya Rais wa Iran anayeitembelea Italia. Vilevile vileo na mvinyo havikuwekwa katika meza ya karamu ya chakula cha usiku iliyotayarishwa na Waziri Mkuu wa Italia kwa ajili ya Rais Hassan Rouhani na ujumbe unaoandamana naye ikiwa ni kuoneesha heshima kwa maadili na sheria za Kiislamu.
Kabla ya kukutana na Waziri Mkuu wa Italia, Rais Hassan Rouhani pia alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo, Sergio Mattarella na vilevile Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani, Papa Francis huko Vatican.
Katika mazungumzo yake ya Papa Francis, Dakta Hassan Rouhani na mwenyeji wake wamesisitiza kuwa lengo la dini za mbinguni ni kueneza amani na kuepusha wanadamu na ukatili na utumiaji mabavu. Vilevile wamesisitza udharura wa walimwengu wote kushirikiana kwa ajili ya kukomesha machungu ya mwanadamu na kusitisha vita na mapigano kote duniani.

0 comments:

Chapisha Maoni