Chelsea wameamua kumfuatilia meneja wa Stoke City Mark Hughes, wakitafuta meneja wa kudumu Stamford Bridge (Guardian), hata hivyo meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino pia ametajwa kuweza kumrithi Jose Mourinho Chelsea (Independent), meneja wa Bournemouth Eddie Howe na Claudio Ranieri wa Leicester pia wametajwa kuwa na uwezekano wa kupewa kazi Stamford Bridge (Daily Telegraph), beki wa Chelsea Gary Cahill, 30, anataka kuodoka Chelsea kutokana na kutopangwa na Guus Hiddink, na ana wasiwasi huenda akakosa kuitwa Euro 2016 (Daily Telegraph) hata hivyo Cahill huenda asiruhusiwe kuondoka Chelsea mwezi huu (Guardian), Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy, 29, na huenda wakampeleka Loic Remy Leicester kama sehemu ya mkataba (Daily Mirror), Chelsea pia wanakarbia kukamilisha usajili wa beki wa New York Red Bulls, Matt Miazga, 20 kwa pauni milioni 3.5, na pia bado wanamfuatilia Aymen Abdennour waliyemkosa na akasajiliwa na Valencia kwa pauni milioni 22 kutoka Monaco (The Times), mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski, 27, atakataa kwenda Manchester City, Manchester United na Chelsea, na atasubiri kuitwa na Real Madrid mwishoni mwa msimu ujao adhabu yao ya kutosajili itakapokwisha (Independent), Leicester wametoa pauni milioni 14 kumtaka mshambuliaji kutoka Nigeria Ahmed Musa, 23, anayeichezea CSKA Moscow, lakini klabu hiyo inataka pauni milioni 19 (Times), Leicester huenda wakaamua kumtaka mshambuliaji wa Southamton Graziano Pelle, 31, kabla ya dirisha la mwezi huu la usajili kufungwa na anaweza kupatikana kwa pauni milioni 5 (Sun), Arsenal wamekubaliana na Dynamo Kiev kumsajili mshambuliaji Andyiy Yarmolenko, 26, kwa pauni milioni 23. Mchezaji huyo alikuwa akinyatiwa na Everton (Sport.ua), Arenal pia wanataka kumsajili mshambiliaji wa Celta Vigo, Nolito, 29, baada ya uhamisho wake kwenda Barcelona kushindikana (Sport), mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, 29, huenda akarejea Liverpool kabla hajastaafu, kwa mujibu wa Brendan Rodgers (Talksport), mchezaji chipukizi wa Feyenoord Tahith Chong, 16, amesema Manchester United wanataka kumsajili, lakini yeye hana mpango wa kuondoka Uholanzi (FR12), Porto wanataka pauni milioni 38 kumuuza Gianelli Imbula, 23, ambaye Stoke City inamtaka lakini imetoa nusu ya kiasi hicho (LeSport10), beki wa Sunderland Sebastian Coates, 25, huenda akajiunga na Sporting Lisbon kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili kufungwa (Sunderland Echo), mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Liverpool Fernando Torres, 31, ataondoka Atletico Madrid alipokuwa akicheza kwa mkopo kutoka AC Milan mwisho wa msimu baada ya kocha Diego Simione kukataa kumpa usajili wa kudumu (Daily Mail), Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 4 kumsajili beki wa Leicester Ben Chilwell, 19 baada ya pauni milioni 3 za awali kukataliwa (Sun), mmiliki wa West Brom Jeremy Peace atakataa kumuuza mshambuliaji Saido Berahini, 22 katika dirisha la usajili la Januari, lakini atakuwa tayari kufanya hivyo mwisho wa msimu (Daily Mirror). Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye baadhi ya magazeti ya Ulaya.
SALIM KIKEKE
0 comments:
Chapisha Maoni