Alhamisi, Januari 28, 2016

30 WAOKOKA KIFO BAADA YA KIVUKO CHA KILOMBERO KUZAMA

WATU wapatao 30 wameokolewa mpaka sasa baada ya kivuko cha Mto Kilombero kushindwa kuhimili upepo mkali ulioambatana na mvua ya radi na kisha kugonga nguzo za pembeni ya mto na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka ndani ya maji.
Tukio la kivuko hicho cha Mto Kilombero kushindwa kumudu upepo sio mara ya kwanza kujitokeza katika eneo hilo la mpakani mwa Wilaya za Kilombero na Ulanga, ambapo juzi hali kama hiyo ilijitokeza pia.

0 comments:

Chapisha Maoni