Jumapili, Januari 24, 2016

HOMA YA 'ZIKA' YAENDELEA KUSAMBAA EQUADOR

Watu 17 wamepata maradhi yanayoenezwa na mbu ya virusi vya Zika nchini Equador, Waziri wa Afya nchini humo,Guevara,amesema.
Waziri Guevara, amewaonya wanawake wote dhidi ya kupata mimba kwa Kuwa Virusi hivyo vinasababisha ulemavu miongoni mwa watoto wadogo wanaozaliwa.
Watafiti wamesema kuwa hali ya hewa yenye unyevu mkubwa ndiyo iliyochangia pakubwa mlipuko wa maradhi hayo.
Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema kwamba karibu mataifa kumi ya Afrika, Asia na Pacific pia yametangaza mlipuko wa maradhi hayo ya Zika.

0 comments:

Chapisha Maoni