Nyota inazidi kung'aa kwa Tanzania, baada ya Mwana Samatta kuipeperusha bendera ya Tanzania jana nchini Ubelgiji na kusaini mkataba wa miaka minne na timu ya FC Genk inayocheza ligi kuu nchini humo, Taarifa tuliyoipata leo ni kwamba mwanamuziki wa Tanzania, staa Diamond Plutnumz ameshinda tuzo mbili usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria.
Diamond amefanikiwa kushinda tuzo hizo mbili katika mashindano mawili tofauti ya Too Xclusive Awards ambapo amechukua tuzo ya Msanii Bora Afrika na katika mashindano ya Trends Loaded ameshinda tuzo ya Msanii Bora Afrika.
Kupitia ukurasa wake wa facebook Diamond ameandika kuwa
"Ningpenda niwashkuru na kuwajuza mashabiki zangu pendwa kuwa kinana wenu nimeshinda tunzo zingine mbili kama MSANII BORA AFRICA kwenye tunzo za #tooxclusiveawards na pia MSANII BORA WA AFRICA kwenye tunzo za TrendsLoaded.... sina cha kuwalipa zaidi ya kuhakikisha nawapatia kazi bora kila nitoapo, kuwawakilisha vyema na kiwaombea kwa Mwenyez Mungu awafanikishie kwenye kila jema mliombalo kwenye Maisha yenu"
Jus wanna thank my people and let you know that have won another two awards in Nigeria AFRICAN ARTIST OF THE YEAR on...
Posted by Diamond Platnumz on Friday, 29 January 2016
0 comments:
Chapisha Maoni