Taasisi inayosimamia utabiri wa hali ya hewa nchini China imetoa tahadhari ya rangi ya machungwa kuhusu wimbi la baridi ambalo linazidi kutanda katika maeneo mbali mbali nchini humo, hii ikiwa ndio nyuzi ya chini zaidi ya baridi kurekodiwa kwa miongo nchini China. Taasisi hiyo hutumia rangi aina nne kuashiria hali ya anga. Rangi ya nyekundu hutumiwa kutoa tahadhari ya hali hatari ya anga, ikifuatwa na rangi ya machungwa, manjano na bluu.
0 comments:
Chapisha Maoni