Jumatatu, Januari 05, 2015

WANANCHI IRINGA WAMESHAURIWA KUSALIMISHA KWA POLISI SILAHA WANAZOZIMILIKI KINYUME CHA SHERIA.

Ili kupunguza ongezeko la vitendo vya uhalifu unaohusisha silaha wananchi mkoani Iringa wameshauriwa kusalimisha kwa jeshi la polisi silaha zao wanazozimiliki kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema kuwa ni vyema wananchi wanaomiliki silaha bila kibali wakazisalimisha katika vituo vya polisi au kwa viongozi wa serikali za mitaa.

Ameongeza kuwa kwa sasa jeshi la polisi mkoa wa Iringa limeanzisha msako mkari wa kuhakikisha kuwa linawakamata watu wote wanaomiliki silaha pasipo kuwa na kibari hali itakayo pelekea wananchi wa mkoa wa Iringa kuishi kwa usalama kwa maisha yao pamoja na mali zao.

Kamanda Mungi amesema kuna baadhi ya wananchi ambao wanamiliki silaha ambazo wamezirithi kutoka kwa ndugu zao ambapo amewataka kufuata taratibu za husika za kisheria ili kupata kibari cha umiliki wa wa silaha hizo.

Aidha amesema licha ya kuwepo kwa wananchi wanaomilili silaha kinyume cha sheria pasipo kuwa na kibari maalumu pia ameongeza kuwa kuna tatizo la baadhi ya wanaomiliki kihalari silaha hizo wanazitumia kwa matumizi ya kihalifu.
 
Hata hivyo, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kuwabaini watu wote wanao miliki silaha bila kibali maaalumu ikiwa ni pamoja kuwafichua wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu hasa wa kutumia silaha za moto

0 comments:

Chapisha Maoni