Jumatano, Oktoba 08, 2014

UHURU KENYATTA MAHAKAMANI ICC LEO

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekuwa rais wa kwanza aliye madarakani kufika mbele ya mahakama ya Kimataifa ya ICC. Bwana Kenyatta anakanusha mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinaadam kuhusiana na madai ya kuhusika kwake katika ghasia za baada ya uchaguzi miaka saba iliyopita. Sababu ya shauri mahakamani siku ya Jumatano, ni kutazama iwapo kesi hiyo iendelee au itupiliwe mbali. Upande wa mashtaka umetaka kesi hiyo iahirishe kwa muda usiojulikana mpaka pale serrikali ya Kenya itakapowasilisha kile inachosema nyaraka muhimu. Upande wa utetezi unasema Bwana Kenyatta hana sababu ya kupanda kizimbani kwa sababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi yake. Uamuzi kamili unatarajiwa kutolewa baadaye siku zijazo. Picha- Uhuru akiwa mahakamani AP.

0 comments:

Chapisha Maoni