Watu wawili wamefariki Mkoani Iringa katika matukio mawili tofauti likiwepo la mtu mmoja kufariki kwa kuuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mtu/watu wasiofahamika.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Salehe Khamisi umri miaka 18 mkazi wa maeneo ya Igumbilo Manispaa na Mkoa wa Iringa ameuawa na kisha kuporwa pikipiki yake na mtu/watu wasiofahamikana.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa marehemu alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Lugalo Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa na chanzo cha mauaji hayo ni watuhumiwa kujitafutia mali pia jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa kuwatafuta walio husika na tukio hilo.
Aidha katika tukio la pili amesema Linus Mwirafi umri miaka 45 mkazi wa maeneo ya Itimbo wilaya ya kilolo Mkoa wa Iringa amefariki papo hapo kwa kuangukiwa na gari no.T.244 CNK aina ya Isuzu Lori ambalo limepinduka na kuacha njia.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na jeshi la polisi Mkoani Iringa linaendelea kumshikilia dereva wa gari hiyo Bw.Yoktani Kikula umri miaka 25 kwa uchunguzi zaidi pia wito umetolewa kwa wamiliki na madereva wa vyombo vya usafiri kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza sheria za usalama barabarani .

0 comments:
Chapisha Maoni