Jumatatu, Oktoba 06, 2014

PIKIPIKI YAUA STAND KUU MBEYA

Mwendesha pikipiki mmoja aliyefahamika kwa jina la Shukurani Mtafya (20) mkazi wa Nzovwe aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili T.805 BDQ aina ya T-Better amefariki dunia baada ya pikipiki hiyo kuacha njia na kuanguka. 
Ajali hiyo imetokea mnamo tarehe jana majira ya saa 06:00 asubuhi maeneo ya Stand Kuu, kata na tarafa ya Sisimba, jiji na mkoa wa Mbeya. 
Chanzo cha ajali kinachunguzwa. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu. 
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa vyombo vya moto kuwa makini, kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

0 comments:

Chapisha Maoni