Mtembea kwa miguu aliyefahamika kwa jina la Robert Mgala
(21) mkazi wa Ihanda alifariki dunia baada ya kugongwa na gari isiyofahamika
namba zake za usajili lililokuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika jina wala
makazi yake.
Ajali hiyo imetokea mnamo jana majira ya saa 16:00 jioni
huko katika kijiji cha Ihanda, kata ya Ihanda, tarafa ya Vwawa, wilaya ya
Mbozi, mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya/Tunduma. Chanzo cha ajali
kinachunguzwa. Dereva alikimbia mara baada ya ajali hiyo, jitihada za kumtafuta
zinaendelea.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Mbozi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi
mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa madereva na watumiaji wengine
wa vyombo vya moto kuwa makini, kuzingatia sheria na alama za usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Aidha, anatoa wito kwa
yeyote mwenye taarifa za mahali alipo dereva aliyehusika katika ajali hii
azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yake.
0 comments:
Chapisha Maoni