Jumatano, Oktoba 15, 2014

MCHANA SHULE...USIKU DANGURO, MKE WA MTU AKUTWA AKINGONOKA

Danguro hatari linaloendesha shughuli zake katika eneo la shule limefichuliwa baada ya kumnasa mwanamke aliyedai ni mke wa mtu akifanya uzinzi na mtu ambaye hakufahamika mara moja  ambaye hakujulikana jina lakejapokuwa inahisiwa kuwa ni mume wa mtu.
Tukio hilo la aibu ya karne lilijiri ndani ya eneo la shule ya msingi Shekilango, iliyopo Mapambano, Sinza jijini Dar, hivi karibuni ambapo mke huyo wa mtu alikuwa akichepuka.
Wawili hao, baada ya kukamatwa wakifanya ngono hadharani walitiwa kizuizini kabla ya vijana wanaodaiwa kuchukua posho kwa wanaofanyia mambo yao kwenye danguro hilo kuanzisha vurumai ingawa walidhibitiwa huku jamaa aliyekuwa anahudumiwa akitoka nduki.
Akizungumza na Fichuo Tz, mwanamke huyo aliomba asamehewe na kusema kwamba kinachomsababishia kufanya shughuli hiyo ni ugumu wa maisha na kundi la watoto anaowalea ambao baba yao hana ajira.
Baada ya mtandao huu kutaka kuzungumza na mumewe ili kujua kama anafahamu kuwa mkewe anafanya biashara haramu ya kuuza mwili, mwanamke huyo alidai kwamba mumewe hana simu.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisikika akisema: 
Dah! Mngewahi dakika kumi tu, mngemkuta baba wa Kiarabu aliyeingia na mwanamke muda si mrefu, hili danguro linatumiwa usiku kucha, yaani linapoingia giza tu hapa ni balaa hadi asubuhi.
Mwalimu wa zamu, Kilavo Charles, amesema  kuwa suala hilo limeshafikishwa kituo cha Polisi Mabatini ambao waliahidi kulishughulikia.
Ni aibu, asubuhi watoto wanafagia kondom, tunakosa cha kuwaambia, hii ni hatari kwa kweli na tunaomba mamlaka zinazohusika zilifanyie kazi jambo hili
lisema.

0 comments:

Chapisha Maoni