Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Iringa Katika
Matukio mawili tofauti likiwepo la mtu mmoja kushikiliwa kwa tuhuma ya
kukutwa akimiliki silaha kinyume cha sheria.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani
Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema askari wanyamapori wakiwa doria
wamemkamata John Mapunda mkazi wa kijiji cha Mbwileli wilaya ya Iringa
Vijijini Mkoa wa Iringa akiwa na bunduki aina ya SHORTGUN yenye no:66721
akiwa anamiliki bila kibali.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa baada ya uchunguzi wa kina kufanyika
nyumbani kwa mtuhumiwa askari hao walimkuta akiwa na nyama ya swara
yenye uzito wa kilo nne akiwa amezipata kinyume cha sheria.
Adha amesema askari polisi wakiwa doria wamekamata Rahedy Joseph umri
miaka 23 mkazi wa maeneo ya Ipogoro Manispaa na Mkoa wa Iringa akiwa na
madawa ya kulevya aina ya bhangi kete 43 ambazo alikuwa amezihifahi
ndani ya hotpoti la chakula,mtuhumiwa ni muuzaji wa madawa hayo.
Wakati huo huo amesema askari polisi wanaendelea na msako wa kuwatafuta
watu waliohusika tukio la kuvamia kwa nguvu na kufanya ung’anganyi
dukani kwa Heppy Ingasi umri miaka 36 mkazi wa maeneo ya Nduli Manispaa
na Mkoa wa Iringa.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema vitu vilivyoporwa ni simu moja aina ya
tecno,fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni mbili pamoja na vocha za
aina mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni tatu na nusu ambapo
watuhumiwa hao walitumia panga kumshambulia mwenye duka.




0 comments:
Chapisha Maoni