Mtu mmoja mkazi wa lupa aliyefahamika kwa jina la magdalena lena (32) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya akiwa na pombe haramu ya moshi [gongo] ujazo wa lita ishirini na tano [lita 25].
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 08.10.2014 majira ya saa 17:30 jioni huko katika kijiji na kata ya lupa, tarafa ya kipembawe, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya. Aidha, mtuhumiwa huyo amekutwa na mtambo mmoja wa kutengenezea pombe hiyo haramu. Mtuhumiwa ni mtengenezaji na muuzaji wa pombe hiyo.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 08.10.2014 majira ya saa 17:30 jioni huko katika kijiji na kata ya lupa, tarafa ya kipembawe, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya. Aidha, mtuhumiwa huyo amekutwa na mtambo mmoja wa kutengenezea pombe hiyo haramu. Mtuhumiwa ni mtengenezaji na muuzaji wa pombe hiyo.
*********************************************************************************************
Mtu mmoja mkazi wa lupa aliyefahamika kwa jina la kisa mwambene (51) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya akiwa na pombe haramu ya moshi ujazo wa lita tano [lita 05].
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 08.10.2014 majira ya saa 17:45 jioni huko katika kitongoji cha lupa kati, kijiji na kata ya lupa, tarafa ya kipembawe, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya. Mtuhumiwa ni mtengenezaji na muuzaji wa pombe hiyo.
Taratibu za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa zinaendelea.
*********************************************************************************************
Watu wawili wakazi wa makunguru jijini mbeya waliofahamika kwa majina ya 1. Mariam nditi (58) na 2. Jackline john (32) wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya wakiwa na bhangi yenye uzito wa gramu 500 [nusu kilo].
Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 08.10.2014 majira ya saa 16:00 jioni huko makunguru, kata na tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. Watuhumiwa walikutwa na bhangi hiyo waliyokuwa wameificha kwenye mfuko wa kaki baada ya kupekuliwa nyumbani kwao.
*********************************************************************************
Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya wakiwa na dawa ya kulevya aina ya bhangi. Watuhumiwa hao ni pamoja na1. Baraka mawasa (22) mkazi wa makongolosi alikamatwa akiwa na kete 10 za bhangi sawa na uzito wa gramu 50 akiwa ameziweka kwenye mfuko wake wa suruali. 2. Malaki gideoni (23) mkazi wa makunguru alikamatwa akiwa na kete 104 za bhangi sawa na uzito wa gramu 520. Aidha 3. Yasini msafiri (15) mkazi wa mwanyanje – uyole alikamatwa akiwa na bhangi kete 107 sawa na uzito wa gramu 535 kwenye mfuko mweusi wa rambo.
Watuhumiwa hao walikamatwa katika msako uliofanyika mnamo tarehe 08.10.2014 majira ya saa 14:00 mchana na saa 22:00 usiku huko katika maeneo ya stendi ya usangu – uyole jijini mbeya na stendi ya mabasi – makongokosi – chunya.
Watuhumiwa ni watumiaji na wauzaji ya bhangi hiyo, taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia dawa za kulevya [bhangi] pia kuacha kutumia pombe haramu ya moshi [gongo] kwani ni hatari kwa afya ya mtumiaji na ni kinyume cha sheria. Aidha, anatoa wito kwa wananchi na wakazi wa mkoa wa mbeya kutoa taarifa katika mamlaka husika za mtu/watu au mtandao wa watu wanaojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa pombe ya moshi pamoja na bhangi ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.




0 comments:
Chapisha Maoni