Asilimia 60 ya watoto katika wilaya za Chunya, Mbeya vijijini na Kyela mkoani mbeya wanahitaji misaada ya hali na mali kuokoa maisha yao kutokana na kuishi katika mazingira magumu yanayosababishwa na wazazi wao kutozingatia uzazi wa mpango, kutokuwa na uwezo wa kichumi au kuachwa yatima.
Hali hiyo imebainika baada ya shirika lisilokuwa la kiserikali la Tehilah Foundation kufanya utafiti ambao umegundua kadhia inayowapata watoto hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.
Katika kuchukua hatua za kuwasaidia watoto hao, shirika hilo limeamua kuwasomesha baadhi yao huku wale ambao umri wao wa kusoma umepita wakiwaspatia nyenzo za kuwasaidia kufanya shughuli za ujasiliamali.
Kutokana na utafiti huo, mashirika yasiyo ya kiserikali yameombwa kuelekeza nguvu zake vijijini ili kuwanusuru watoto ambao wanakosa huduma muhimu kwa ajili ya kuendelesha maisha yao.

0 comments:
Chapisha Maoni