Jumatatu, Septemba 22, 2014

WANAWAKE UWT IRINGA, HILI SOMO KWENU

Wanawake mkoani Iringa wametakiwa kujishughulisha na kazi za maendeleo ili kuongeza kipato chao hali ambayo itasaidia kutowategemea waume zao.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoani Iringa Bi. Zainabu Mwamwindi amesema kuwa wanawake wakijituma katika kazi za uzalishaji mali ili kuleta maendeleo ya taifa.
Aidha amewataka wanawake kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama na kuondokana na dhana ya kuteuliwa katika viti maalum.
Amewashauri wanawake kuondoa makundi ndani ya chama hususani  katika kipindi cha uchaguzi wa jumuiya hiyo ili kuimarisha umoja na mshikamano.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa UWT mkoani Iringa Bi. Zainabu Mwamwindi ameshauri kuwepo kwa uwajibikaji wa viongozi ndani ya jumuiya hiyo ili kuitekeleza vyema sera ya chama cha mapinduzi CCM.

0 comments:

Chapisha Maoni