Baraza la ardhi na nyumba mkoani Arusha limeamuru mwili wa marehemu Paulina Lucas aliyezikwa katika eneo la mgogoro wa shamba katika kijiji cha Elkiushin ufukuliwe mara moja na kisha ukazikwe kwenye makaburi ya umma .
Amri hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na mwenyekiti wa baraza hilo mkoani hapa ,Cyriacus Kamugisha kufuatia shauri nambari 222 la mwaka 2006 lililofunguliwa na Francis Levava aliyekuwa akiwakislishwa na wakili,Ezra Mwaluko.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo mbele ya pande zote ,Kamugisha alisema kuwa mnamo juni 11 mwaka 2006 mara baada ya shauri hilo kufikishwa mbele ya baraza hilo ilimariwa ya kwamba kisifanyike kitu chochote katika eneo hilo hadi shauri hilo la msingi litakaposikilizwa lakini upande wa wajibu maombi ulikiuka agizo hilo.
Kamugisha,alisema kuwa upande wa mlalamikiwa ambaye ni ,Kerusoi Loilole aliyewakilishwa na wakili Daud Haraka ulikiuka amri ya msingi ya baraza hilo kwa kuzika mwili wa marehemu sanjari na kujenga nyumba na choo katika eneo hilo ihali eneo lina mgogoro.

Kitendo alichokifanya mjibu maombi kuhifadhi mwili wa marehemu hakikuwa sahihi kwani eneo lilikuwa na mgogoro,kitendo hiki ni kudharau amri halali ya mahakama
alisema Kamugisha. Hatahivyo,akisoma hukumu hiyo mwenyekiti huyo alitamka kwamba jengo la choo na nyumba vilivyojenga katika eneo hilo vibomolewe mara moja na kuagiza zoezi hilo linapaswa kusimamiwa na mkuu wa polisi wilayani Arusha(OCD) pamoja na maafisa watendaji wa kijiji na kata katika eneo la mgogoro.
Alisema amri hiyo inapaswa kutekelezwa mara moja kuanzia tarehe ya hukumu na kimsingi maombi ya mleta maombi yanakubaliwa kwa gharama na baraza hilo kufukua mwili wa marehemu huyo.
Alisema amri hiyo inapaswa kutekelezwa mara moja kuanzia tarehe ya hukumu na kimsingi maombi ya mleta maombi yanakubaliwa kwa gharama na baraza hilo kufukua mwili wa marehemu huyo.
Akiongea mara baada ya hukumu hiyo upande wa mlalamikiwa,Loilole alisema kuwa hakumu hiyo haikutenda haki na huenda ikazua maafa kwa kuwa walianza kuzika miili mbalimbali katika eneo hilo tangu miaka ya nyuma hata kabla ya marehemu Lucas.
Kwa upande wa walalamikaji kupitia kwa wakili wake,Mwaluko alisema kuwa wameridhishwa na hukumu hiyo kwani imetenda haki kwani eneo hilo ni mali halali ya mteja wake.
Kwa upande wa walalamikaji kupitia kwa wakili wake,Mwaluko alisema kuwa wameridhishwa na hukumu hiyo kwani imetenda haki kwani eneo hilo ni mali halali ya mteja wake.
0 comments:
Chapisha Maoni