Alhamisi, Septemba 18, 2014

WAKULIMA IRINGA WATAKIWA KUENDANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi wakulima Mkoani Iringa wametakiwa kulima kilimo rafiki na mazingira pamoja na kuyatumia mazao yanayostahimili hali ya ukame.
Afisa afya ya mimea wilaya ya Iringa Mkoani Iringa David Chilagane amesema hali ya ukame nchini na dunia kwa ujumla imetokana na shughuli mbalimbali za viwanda,ufugaji pamoja na kilimo cha kiasilia ambacho huhusisha ukataji miti na kutobadilisha aina ya mazao.
Bw.Chilagane ameongeza kuwa shilika la MMADEA likishilikiana na maafisa mimea na mifugo wilaya ya Iringa Mkoani Iringa  wanaendesha kampeni ya utoaji wa elimu ya kukabiliana na hali hiyo kwa wakulima na wafugaji wanaozunguka vijiji vya Bwawa la Mtera pamoja na vijiji vya Weru na Kibebe.
Aidha amesema elimu hiyo ilianza kutolewa kwa msimu wa kilimo wa 2013-2014 ambapo wanaendelea na maandalizi ya msimu mpya wa kilimo kwa mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuwawezesha pembejeo za dawa na mbegu za kunde,tikiti maji na alizeti ambayo hustahimili ukame.
Hata hivyo Bibi shamba wa kata ya ulanda wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa Bi.Fatuma Ngoma amewaasa wakulima na wafugaji wa wilaya ya Iringa Vijijini wahakikishe wanaitumia elimu hiyo kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuzitumia pemejeo hizo kwa wakati na kuwasaidia wenzao ili waweze kunufaika na elimu hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni