Takwimu za tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) zinaonyesha
kuwa kiwango cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika barabara za
kimataifa kwenye vituo vya kulaza magari ya mizigo ya masafa marefu kiko
juu ikilinganishwa na wastani wa taifa.
Wastani wa juu wa kitaifa wa maambukizi hayo unatajwa kuwa asilimia
5.1 wakati kwenye vituo hivyo ni kati ya asilimia 15 hadi 35.
Mratibu wa Program Maalumu ya TACAIDS Renatus Kihungo ameeleza Sababu
zinazochangia ongezeko hilo na kueleza hatua wanazochukua kudhibiti
hali hiyo kuwa ni pamoja na kuongeza vituo vya kutolea elimu katika
barabara hizo ambavyo sasa vimefika 14.
Pamoja na mambo mengine ametaja baadhi ya huduma zitakazokuwa
zikitolewa katika vituo hivyo kuwa ni pamoja na ugawaji wa kondom,
huduma za ushauri nasaha, upimaji wa hiari, rufaa kwa matibabu maalumu,
unasihi wa upimaji wa VVU na utoaji wa huduma ya habari elimu na
mawasiliano.
Baadhi ya vituo hivyo ni Kagongwa- Kahama, Kibaigwa, Mdaula, Bagamoyo, Uvinza, Kasumulu Kyela na Tunduma Mbozi.
0 comments:
Chapisha Maoni