Alhamisi, Septemba 18, 2014

MTUHUMIWA ADAI KUINGIZIWA MTI SEHEMU ZA SIRI AKIWA MAHABUSU ARUSHA

MSHITAKIWA katika kesi ya ugaidi, Abdallah Maginga, ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kumruhusu kutohudhuria siku za kesi na abaki magereza, kutokana na maumivu makali anayodai anayapata sehemu za siri alikominywa na polisi na kuingiziwa mti kwenye haja kubwa.
Mheshimiwa Hakimu naomba mahakama yako inipe ruhusa ya kutohudhuria siku ya kesi, sababu ninapopanda gari napata maumivu makali sana sehemu za siri kunauma kwa sababu polisi walinitesa kwa kuniingizia mti kwenye haja kubwa na kuminya sehemu zangu za siri
alisema.
Alisema mbele ya Wakili wa Serikali, Rose Sulle kuwa mbali na maumivu ya sehemu za siri, pia mguu wake uliokatwa hospitalini, bado unamsumbua kutokana na maumivu.
Maginga pia aliomba iagize Magereza wamruhusu akatibiwe hospitalini, kwani alitakiwa kwenda kupata matibabu Septemba 5 mwaka huu, ila alizuiwa hadi sasa.
Akijibu hoja hizo, Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo, Devotha Msofe, alisema suala la kuja mahakamani ni lazima na mahakama haiwezi kumpa ruhusa hiyo.
Pia, alimshauri mshitakiwa huyo kuwa kama ana maelezo mengi, amweleze hakimu anayesikiliza kesi yake, Mustapher Siyani ambaye kwa siku hiyo hakuwepo.

0 comments:

Chapisha Maoni