Jumatano, Septemba 17, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Siku kama ya leo miaka 53 iliyopita yaani tarehe 18 Septemba mwaka 1961, aliaga dunia Dag Hammarskjold, mwanasiasa wa Sweden na Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa. Mwanasiasa huyo alifariki dunia baada ya ndege iliyokuwa imembeba kuanguka katika ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hammarskjold alikuwa Congo kwa lengo la kukomesha vita vya ndani. Mwanasiasa huyo alizaliwa mwaka 1905 na alihesabiwa katika zama zake kuwa miongoni mwa waandishi stadi nchini Sweden. Mwaka 1952, Dag Hammarskjold alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel miaka michache baada kuaga dunia.
Na miaka 899 iliyopita katika siku kama ya leo kazi ya kuandika tafsiri mashuhuri ya Majmaul Bayan ilimalizika. Kitabu hicho kiliandikwa na Sheikh Tabarsi mmoja wa wafasiri wakubwa wa Qur'ani Tukufu na miongoni mwa maulamaa mashuhuri wa Iran aliyekuwa mashuhuru kwa jina la Aminul Islam kutokana na uaminifu na uchamungu wake. Kitabu hicho ni miongoni mwa tafsiri mashuhuri za Qur'ani kutokana na mbinu yake ya kuvutia katika mtazamo wa fasihi. Tafsiri hiyo imechapishwa mara kadhaa katika nchi za Iran, Lebanon na Misri.

0 comments:

Chapisha Maoni