Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amemteua muigizaji wa Marekani, Leonardo Dicaprio kuwa mjumbe wa amani wa umoja wa mataifa atakaesaidia kuhamasisha hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumanne, Ban Ki-moon alisema kuwa muigizaji huyo sio tu kuwa ni moja kati ya waigizaji wanaoongoza duniani lakini pia amekuwa akijikita kwa muda mrefu katika shughuli za mazingira.
Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa aliongeza kuwa, Jumanne ijayo DiCaprio atahutubia mkutano wa mazingira na tabia nchi unaotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa juu wa mataifa 120.
Leonardo DiCaprio alianzsha foundation yake mwaka 1998 iliyojikita katika mpango wa kuhamasisha matumizi bora ya mazingira na uhusiano mzuri kati ya binadamu na dunia asilia.
Muigizaji huyo anaungana na watu 11 maarufu duniani wanaofanya kazi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kama wajumbe wa amani. Wengine ni Stevie Wonder, Michael Douglas, George Clooney, Paula Coelho ambaye ni mwandishi kutoka Brazil na Daniel Barenboim.
0 comments:
Chapisha Maoni