Jumatatu, Septemba 15, 2014

SHIRIKA LA HAKI ZA BINADAMU LAWATETEA WAATHIRIKA WA EBOLA

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limezitaka nchi za Kiafrika za Liberia, Guinea na Sierra Leone ambazo zimeathiriwa zaidi na maradhi ya Ebola kuheshimu haki za kimsingi za binadamu.
Takwa hilo la HRW limetolewa katika hali ambayo, Sierra Leone imewataka wananchi wote kubaki majumbani mwao mwishoni mwa wiki hii kuanzia tarehe 19 hadi 21 Septemba. Viongozi wa Liberia pia wanatuhumiwa kuweka karantini zisizo za kisheria na zinazokiuka uhuru wa mwanadamu. Taarifa iliyotolewa na Human Rights Watch imewakosoa viongozi wa nchi hizo kwa kuweka karantini na kuwapiga marufuku watu kutembea katika baadhi ya maeneo na vijiji bila ya sababu za kitaalamu na kimsingi.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya watu 2,300 wamepoteza maisha kutokana na maradhi ya Ebola yaliyolikumba zaidi eneo la Magharibi mwa Afrika.

0 comments:

Chapisha Maoni