Mahakama ya Misri imemuhukumu Muhammad Badie Kiongozi wa Harakati ya
Ikhwanul Muslimiin iliyopigwa marufuku na wanachama wengine 14 wa
harakati hiyo adhabu ya kifungo cha maisha jela baada ya eti kuwapata na
hatia ya kufanya mauaji na uchochezi katika eneo lililoko karibu na
Cairo mji mkuu wa Misri.
Jaji wa Mahakama hiyo aliitisha kesi hiyo kwa lengo la kusikiliza maelezo ya mashahidi, lakini aliamua kutoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa watuhumiwa hao. Muhammad Badie mwenye umri wa miaka 71 ni miongoni mwa mamia ya wanachama wa Ikhwanul Muslimin ambao tayari wamehukumiwa adhabu ya kifo, hukumu ambayo imekosolewa vikali na makundi ya kutetea haki za binadamu duniani.
Tangu ilipoondolewa madarakani serikali ya Rais Muhammad Morsi mwezi Julai mwaka jana, kwa akali watu 1,400 wameuawa, 15,000 wametiwa mbaroni, huku 200 kati yao wakihukumiwa adhabu ya kifo.

0 comments:
Chapisha Maoni