Umoja wa Afrika AU umetuma timu ya wataalamu 30 na wauguzi katika
nchi za Afrika magharibi ili kusaidia kuzuia kueneza virusi vya ugonjwa
wa Ebola katika nchi zilizoathirika.
AU imeeleza kuwa timu hiyo ya
waliojitolewa kwenda kwenye nchi zilizoathiriwa na Ebola inajumusha
wataalamu wa magonjwa ya mlipuko, tiba, wataalamu wa afya ya umma na
afisa mawasiliano.
Imepangwa kuwa timu hiyo itaanza kufanya kazi nchini
Liberia tarehe 17 mwezi huu wa Septemba ambapo pia kundi la pili la
wataalamu litaelekea nchini Sierra Leone wiki ijayo.
Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya unafanya mkutano mjini Brussels
unaowakutanisha mawaziri na maafisa wa ngazi za juu kwa lengo la
kushirikiana na Umoja wa Afrika katika kukabiliana na ugonjwa hatari wa
Ebola.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya watu 2,300
wamekwishapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo, huko magharibi mwa
Afrika.
0 comments:
Chapisha Maoni