Rais Barack Obama wa Marekani
ametishia kuiangusha serikali ya Syria iwapo Rais Bashar Asad ataamuru
kutunguliwa ndege za kijeshi za Marekani na waitifaki wake katika anga
ya nchi hiyo na hii nimeinukuu katika gazeti la New York Times kwaajili yako msomi wa Fichuo Tz.
Marekani na waitifaki wake wa Ulaya na Mashariki ya Kati
zinajiandaa kuanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la kigaidi la
Daesh ndani ya ardhi ya Syria bila ya kupata idhini kutoka kwa serikali
halali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Asad.
New York Times limemnukuu
afisa mwandamizi wa Ikulu ya White House akisema kuwa, Obama ataamuru
kuharibiwa kabisa mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria na kuipindua serikali
ya Damascus iwapo ndege za kijeshi za Washington zitaangushwa na jeshi
la Syria.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Walid al-Mualim alisema
majuma kadhaa yaliyopita kuwa, Syria inakaribisha nchi yoyote inayotaka
kushambulia magaidi katika ardhi yake lakini mashambulizi hayo sharti
yafanyike kwa ushirikiano na Damascus.
Katika kujibu kauli hiyo, Waziri
wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, amesema Washington haitaomba
idhini ya Damascus ili kuingia kijeshi Syria na kushambulia magaidi wa
Daesh.
0 comments:
Chapisha Maoni