Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa mlipuko wa homa ya ebola
ulioziathiri baadhi ya nchi huko magharibi mwa Afrika umeua watu zaidi
ya 2500 hadi hivi sasa huku wengine zaidi ya 5000 wakiambukizwa virusi
hatari vya maradhi hayo.
Bruce Aylward, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Afya Duniani amesema kuwa ni vigumu kutoa makadirio sahihi kuhusu
idadi ya watu wanaoweza kuambukizwa virusi vya ebola, lakini akasema
kuwa idadi ya wanaoambukizwa inaweza kuwa makumi ya maelfu iwapo
kutakuwa na radiamali ya haraka ya kuzuia kuenea haraka kwa virusi vya
ugonjwa huo.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa dola karibu bilioni moja
zinahitajika ili kukabiliana na mlipuko wa virusi vya ebola uliojitokeza
mwezi Machi mwaka huu huko magharibi mwa Afrika.
0 comments:
Chapisha Maoni