Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na
Benki ya Dunia zimetahadharisha kuwa ukosefu wa fedha za kutosha kwa
ajili ya ujenzi mpya wa Ghaza unaweza kusabababisha machafuko zaidi
kati ya Wapalestina na utawala wa Israel.
Benki ya Dunia imesema kuwa
bila ya hatua za haraka za kufufua uchumi na kuboresha anga ya biashara,
kurejea katika machafuko huko Ghaza kama ilivyoshuhudiwa katika miaka
ya hivi karibuni kutasalia kuwa hatari ya wazi.
Wakati huo huo IMF imechapisha ripoti
Jumanne hii ikitilia mkazo kufanyika juhudi ili kupunguza mzingiro wa
kiuchumi wa miaka saba uliowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko
Ukanda wa Ghaza.
IMF imeongeza kuwa iwapo Israel haitaondoa mzingiro
wake huko Ghaza ikiwemo kuruhusu vifaa vya ujenzi kuingizwa katika eneo
hilo, basi juhudi za ujenzi mpya zitakwama.
0 comments:
Chapisha Maoni