Jumanne, Septemba 16, 2014

SENETI YA NIGERIA YATAKA IANZISHWE VITA KUU NA BOKO HARAM

Seneti ya Nigeria imemtaka Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo kuanzisha vita vya pande zote na kundi la kitakfiri la wanamgambo wa Boko Haram. Wawakilishi wa bunge la Seneti la Nigeria wamemtaka Rais wa nchi hiyo kuanzisha vita vya kweli dhidi ya kundi la wanamgambo wa Boko Haram ili kulizuia kundi hilo kusonga mbele huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. David Mark, Spika wa Seneti ya Nigeria amesema  wanamgambo wa Boko Haram wametangaza vita dhidi ya nchi hiyo na kwa msingi huo kundi hilo halipasi kuchukuliwa kama kadhia inayohusiana na usalama wa ndani, bali Nigeria pia  inapasa kutangaza vita dhidi ya kundi hilo.

0 comments:

Chapisha Maoni