Jumanne, Septemba 16, 2014

IRUWASA-IRINGA YANENA NA WATUMIAJI WA MAJI

Mamlaka ya maji safi na maji taka Manispaa ya Iringa (IRUWASA) imewaasa wananchi kuwa makini na uunganishaji kinyemela kwenye mtandao wa huduma hiyo.
Msimamizi Mkuu kitengo cha maji taka na usafi wa mazingira kutoka mamlaka ya maji safi na maji taka Mkoani Iringa (IRUWASA) Mkoani Iringa Bw.Yohana Bugando amesema kumekuwa na ongezeko la wananchi wanaounganishwa huduma ya maji safi na taka kwa kutumia mabomba feki na mafundi ambao hujitambulisha kama wametumwa na mamlaka hiyo.
Bw.Bugando ameongeza kuwa hali hiyo hupelekea kupotea kwa maji kwa kupasuka na kuvuja maji mitaani kutokana na kuunganishwa kwa mabomba yasiyo imara na mafundi walaghai pia IRUWASA kutonufaika na huduma ya kutolipwa kwa ghalama za kila mwezi za utumiaji wa huduma ya maji hayo.
Aidha amewaasa wananchi kufuata utaratibu wa kuunganishwa huduma ya maji kwa kutuma maombi kwa uongozi wa serikali za mitaaa,maafisa ardhi wa eneo husika na hatimaye mamlaka ya IRUWASA ndiye mwenye mamlaka ya kutoa huduma ya uunganishaji wa mtaandao wa maji safi na taka.
Hata hivyo,Bw.Bugando amesema IRUWASA inaendelea na mpango wa kuhakisha wakazi wa kata za Ilala,Makorongoni,Mivinjeni pamoja na Gangilonga Manispaa ya Iringa wanaunganishwa na huduma ya maji taka hivyo wananchi waepuke kutupa vitu vigumu na mchanaga kwenye mabomba ya maji taka.

0 comments:

Chapisha Maoni