Jumanne, Septemba 16, 2014

POLISI IRINGA WAHAHA KUMSAKA MWIZI WA SANLG

Jeshi la polisi Mkoani Iringa linaendelea na uchunguzi pamoja na msako wa kumtafuta mtu mmoja anayefahamika kwa sura kwa tuhuma ya kuiba pikipiki chanzo chake kikiwa ni tamaa ya kumiliki mali.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema pikipiki yenye namba za usajili T; 610 DAQ aina ya SunLG ni mali ya Salum Ngoda umri miaka 28 mfanya biashara na mkazi wa eneo Zizi la ng’ombe Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.
Hata hivyo Kamanda Mungi ameongeza kuwa tukio hilo limetokea Sept 15 mwaka huu eneo la Mshindo Manispaa ya Iringa aidha ametoa wito kwa wamiliki wa pikipiki na madereva bodaboda kuwa makini na uhifadhi pamoja na maegesho ya vyombo hivyo vya usafiri ili kupunguza vitendo vya wizi wa pikipiki.

0 comments:

Chapisha Maoni