Mtoto aliyefahamika kwa jina la Paston Majuto aliye na miaka 9 amefariki dunia baada ya kugongwa na gari jana majira ya saa tatu asubuhi huko Inyara, Wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya gari aina ya Toyota Hiece lenye namba za usajili T.481 ABF lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Kudra Bakari mwenye miaka 44 mkazi wa Soweto hapa jijini Mbeya kumgonga mtembea kwa miguu, mtoto Paston Majuto aliye na miaka 9 tu ambaye ni mkazi wa Inyala, Mbeya Vijijini mkoani Mbeya na kisha kufariki papo hapo.
Imefahamika kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari lililosababisha kifo cha mtoto huyo ambapo baada ajali hiyo kutokea mwili wa marehemu ukahifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya na dereva amekamatwa pamoja na gari lililosababisha ajali hiyo.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoani Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini watumiapo vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia ama kufuata sheria za usalama wa barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kuepukika.

0 comments:
Chapisha Maoni