Alhamisi, Septemba 18, 2014

DOKII ATOA RUSHWA YA MAHABA KWA ASKARI BARABARANI

Mwigizaji wa kitambo na mwimbaji wa muziki wa Kizazi Kipya, Ummy Wenslaus 'Dokii' anadaiwa kutoa kali ya karne baada ya kumpa askari wa jiji rushwa ya busu, Ijumaa lina mkanda kamili. Tukio hilo lilijiri kwenye Makutano ya Mtaa wa Narung’ombe na Swahili, Kariakoo jijini Dar, asubuhi ya saa 4:00, Septemba 15, mwaka huu.
Kwa mujibu wa ‘shushushu’ wetu, Dokii alipaki ‘vibaya’ gari alilokuwa nalo aina ya Toyoya Noah la rangi nyeusi ambapo alifuatwa na kuambiwa kwamba sehemu aliyopaki hairuhusiwi.
Ilisemekana kwamba alitumia ‘ustaa’ wake kuwapuuza akaingia kwenye maduka na kuendelea na ‘shopping’ zake.Ilidaiwa kwamba aliporudi na kutaka kuondoka, alikuta mkoko huo umefungwa mnyororo na vyuma kwenye tairi la nyuma na askari wa jiji (city parking) hivyo akashindwa kutimua.
Ilielezwa kwamba baadaye alifuatwa na mkuu wa askari hao almaarufu kwa jina la Masai ambaye alimwambia kuwa alitakiwa kutoa faini ya shilingi elfu hamsini.
Iliendelea kudaiwa kwamba huku akidhani watu hawamjui alilianzisha na askari hao na kuanza kuzozana.
Muda mfupi baadaye ilijitokeza kadamnasi ambayo ilikuwa ikimzomea ndipo akakimbilia dukani kwa mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Chid.
Ilidaiwa kwamba mwanaume huyo alimpatia msanii huyo shilingi elfu tano ili awapoze askari hao huku akimuombea wamfungulie gari aondoke lakini jamaa hao waliikataa.
Ilielezwa kwamba baada ya kuomba sana askari hao walikubali kumwachia baada ya kummwagia kiongozi wao mabusu ya kimahaba hadharani, kisa tu hakuwa na fedha ya kulipa faini.
Ilidaiwa kwamba baada ya kumlainisha jamaa huyo kwa mabusu motomoto na kufutiwa shitaka, aliachiwa huru bila kutoa chochote huku askari aliyeonjeshwa ‘utamu’ akibaki na mfadhaiko huku akiomba namba ya simu.
Ilisemekana kwamba ili kuua msala, msanii huyo alimpatia namba ya simu kisha akatoka nduki.

0 comments:

Chapisha Maoni