Alhamisi, Septemba 18, 2014

BODABODA YAUA MBEYA

Mtu mmoja amekutwa na mauti wakati akiendesha pikipiki jijini Mbeya mara baada ya kugongwa na gari ambalo halikutambulika katika maeneo ya njia panda ya Moondust, kata ya Ruanda jana majira ya saa mbili usiku.
Taarifa toka kwa maafisa wa polisi mkoani Mbeya imeeleza kuwa mtu huyo aliyefariki dunia hakufahamika kwa jina mara moja baada ya tukio lakini anakadiriwa kuwa ni kijana mwenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 23 ambaye mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Taarifa hiyo imekwenda mbele zaidi na kueleza kuwa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mpaka sasa lakini dereva aliyesababisha ajali hiyo alitokomea kusikojulikana mara tu baada ya tukio na jeshi la polisi mkoani hapa bado linaendelea na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa huyo.
Nae kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutukia kwa tukio hilo na kutoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa vyombo vya moto kuwa makini, kuzingatia na kufuata sheria na alama za usalama barabarani ilki kuepuka ajali, lakini pia ametoa wito kwa yeyote aliye na taarifa za mahali alipo mtuhumiwa yaani dereva wa gari hilo azitoe ili sheria ichukuliwe dhidi yake.

0 comments:

Chapisha Maoni