Habari za kuaminika kutoka Jamhuri Kidemokrasia ya Kongo zinasema
kuwa, kwa karibu askari polisi wawili wameuawa na wengine kujeruhiwa,
baada ya kujiri mapigano makali kati askari polisi na wanajeshi wa Kongo
katika jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo.
Afisa mmoja wa jeshi la Kongo amesema kuwa, mapigano hayo yametokea
baada ya Brigedi nambari 601 ya jeshi kufanya shambulio la kushtukiza
dhidi ya doria ya askari polisi waliokuwa wakifanya uporaji katika mji
wa Kichanga, ulioko umbali wa kilomita 60 kaskazini mwa Goma, makao
makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini.
Duru za kijeshi kutoka Goma zimethibitisha kutokea mapigano hayo na
askari wawili wa jeshi la polisi kuuawa. Inafaa kuashiria hapa kuwa,
eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kongo linakabiliwa na machafuko na
mapigano ya mara kwa mara yanayosababishwa na baadhi ya makundi ya
waasi.
0 comments:
Chapisha Maoni