Ijumaa, Agosti 15, 2014

WATU 50 NA MBUNGE MMOJA KUFA KWA EBOLA NCHINI

Nabii wa Kanisa la Ufunuo kwa Watu Wote lililopo eneo la Yombo Buza-Kipera jijini Dar, Yaspi Paul Bendera ametoa utabiri kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Ebola hapa nchini akizungumza na waandishi wa habari.
Katika utabiri wake, Nabii Yaspi amesema watu 50 watapoteza maisha kwa ugonjwa huo, wakiwemo madaktari wawili na mbunge mmoja.
Nabii huyo amesema kuwa kwa sasa ugonjwa huo bado haujaingia nchini lakini unaweza kuingia muda wowote kuanzia sasa iwapo watu wataendelea kutomtii Mwenyeji Mungu.

0 comments:

Chapisha Maoni