Siku kama ya leo miaka 54 iliyopita, nchi ya Jamhuri ya Congo Brazzaville ilifanikiwa kujipatia uhuru wake kutoka kwa mkoloni Mfaransa. Awali Congo Brazzaville ilikuwa sehemu ya Congo Magharibi iliyojumuisha Zaire ya zamani na Angola. Congo Brazzaville yenye ukubwa wa kilomita mraba 342, 000 inapakana na nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cameroon, Gabon, Jamhuri ya Kidemokorasia ya Congo na Angola.
Siku kama ya leo miaka 24 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 24 Mordad 1369 Hijria Shamsia, Saddam Hussein Rais wa zamani wa Iraq alimtumia barua Hujjatul Islam Walmuslimin Hashemi Rafsanjani aliyekuwa Rais wa Iran kwa wakati huo, akimjulisha kwamba amekubali kikamilifu vipengee vya makubaliano ya mpaka yaliyotiwa saini 1975 nchini Algeria. Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 27 Shahrivar 1359 Hijria Shamsia, Saddam Hussein baada ya kushawishiwa na madola ya kibeberu ya Magharibi, alijitokeza kwenye televisheni ya Iraq na kuuchanachana mkataba huo, na baada ya siku chache, alianza kuivamia ardhi ya Iran. Saddam Hussein na waitifaki wake walidhani kwamba, muda mfupi tu baada ya kuivamia ardhi ya Iran wangeliweza kuuangusha mfumo wa Kiislamu hapa nchini. Hata hivyo mapambano ya wapiganaji shupavu wa Iran yalibatilisha njama zao na jeshi vamizi la Iraq likalazimika kurejea nje ya mipaka ya Iran.
Na siku kama ya leo miaka 9 iliyopita, yaani 15 Agosti 2005, utawala wa Kizayuni wa Israel ulilazimika kuondoka kwenye eneo la Ukanda wa Gaza- magharibi mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Eneo hilo lilitekwa na kukaliwa kwa mabavu na wanajeshi wa Israel kwenye vita vya Waarabu na utawala huo ghasibu mwaka 1967. Hata hivyo, utawala huo wa Israel bado unaendeleza uchokozi na mauaji ya wananchi wasio na hatia wa Palestina katika eneo la Ukanda wa Gaza.

0 comments:
Chapisha Maoni