Jumanne, Agosti 05, 2014

SONGEA WATAFUTA NAMNA YA KUUZA MAHINDI YAO KENYA

Wakati uzalishaji wa mahindi katika mkoa wa Ruvuma mwaka huu ukikadiliwa kuwa tani zaidi ya laki nne uhakika wa soko hilo umekuwa mdogo hivyo wakulima wa mkoa wa Ruvuma wamekutana kujadiliana namna ya kupeleka mahindi yao kuuza nchini Kenya.
Katika kikao hicho amabacho wakulima wa Songea wameteua ujumbe wa watu wanne kwenda nchini Kenya kuzungumza namna mauziano ya mahindi yatakavyokuwa, afisa biashara wa halmashauri ya wilaya ya Songea ambayo ndiyo mzalishaji mkubwa wa mahindi kwa mkoa wa Ruvuma Bw. Furaha Mwangakala amesema kuwa soko la mahindi hakuna hivyo amewataka wakulima kuchangamkia soko la Kenya ambayo imeahidi kununua tani  za mahindi laki mbili na elfu nane nchini.
Kufuatia maelezo hayo wakulima mkoani  Ruvuma wameilaumu serikali kwa kuhimiza kilimo kwanza hususani katika mahindi wakati soko la uhakika hakuna kutishia kugoma kulima huku pia wakiilaumu serikali kwa kulipishwa ushuru wa mazao mara mbili hali inayowafanya kukosa soko la mahindi toka nchi za jirani ambazo zimekuwa zikinunua mahindi  mikoa mingine.

0 comments:

Chapisha Maoni