Jumanne, Agosti 05, 2014

BUNGE LA KATIBA LAANZA BILA UKAWA

Nchini Tanzania leo Bunge Maalumu la Katiba linaendelea na vikao vyake mjini Dodoma katika mchakato mzima wa kutafuta katiba mpya. Bunge hilo linarejea vikao vyake baada ya kikao cha kwanza kuahirishwa kwa ajili ya kupisha vikao vya bunge la bajeti.
Hata hivyo kundi linalojiita Katiba ya Wananchi, au UKAWA kwa ufupi, halihudhurii vikao vya sasa likisema mapendekezo ya wananchi hayajumuishwi katika mchakato huo, hasa kupuuziwa kwa muundo wa serikali tatu kama ulivyopendekezwa na Rasimu ya Katiba.

0 comments:

Chapisha Maoni