UPANDE wa Jamhuri umeiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
ilitupe ombi la Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh
Ponda Issa Ponda la kuitaka itoe amri ya kusimamisha usikilizwaji wa
kesi ya msingi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro,
kwa sababu lina dosari kisheria.
Maombi hayo yaliwasilishwa jana na Wakili Mwandamizi wa Serikali,
Bernad Kongora, mbele ya Jaji Lawrence Kaduri, wakati ombi hilo
lilipokuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
Hata hivyo, ombi hilo la msingi lilishindwa kuanza kusikilizwa kwa
sababu upande wa jamhuri ulikuwa umewasilisha pingamizi la awali la
kutaka litupwe, ambapo jana mahakama hiyo ilianza kusikiliza pingamizi
hilo.
Ponda anaiomba mahakama itoe amri ya kusimamishwa usikilizwaji wa
kesi ya uchochezi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro
hadi rufaa yake iliyokatwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
itakapomalizika.
Wakili Kongora alisema kuwa wanaomba ombi hilo litupwe kwa kuwa hati
ya kiapo na chemba samansi zina dosari kisheria ambazo hazirekebishiki.
Alidai kuwa mwaka 2012-2013 Ponda alishitakiwa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, akahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje na Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, hakuwepo katika Mahakama ya Kisutu na sheria
Na.3 ya mwaka 2011, inaelekeza wazi jinsi utaratibu wa kuandika hati za
viapo.
Alidai kuwa aya ya tano na sita ya ombi hilo la Ponda anayetetewa na
Wakili Nassor Juma, zina maombi ambayo hawatakiwi kuweka kwenye hati ya
kiapo.
0 comments:
Chapisha Maoni