Wema Sepetu ametangaza dau la shilingi milioni moja kwa yeyote
atakayefanikisha kupatikana kwa mbwa wake aitwae Vanila aliyepotea hivi
karibuni.
Akielezea ishu hiyo, Wema alisema mbwa huyo alikuwa na mwenzake
akiishi nao nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo
juzikati alikorofishana na mwenzake aitwae Thiona na kuamua kutokomea
kusikojulikana.
Msanii huyo alisema anaomba yeyote atakayemuona Vanila
wake awasiliane naye au atoe taarifa kituo chochote cha polisi kilicho
karibu naye na atakabidhiwa pesa zake taslimu.




0 comments:
Chapisha Maoni