Jumapili, Agosti 03, 2014

MAPRODUCER WAMTIMUA DIAMOND

Nyota wa muziki wa Bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’, amesema licha ya kutafuta video zenye kiwango, pia dharau na mapozi ya watayarishaji wengi wa Tanzania yamechangia kuacha kutengeneza kazi zake nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi kabla ya kwenda nchini Canada, Diamond alisema mtayarishaji unalipa hela kwanza ndio anakufanyia kazi zako, lakini watayarishaji wa hapa nchini ukishawalipa, kinachofuata ni usumbufu katika kukamilisha kazi.

Siwezi kumlipa mtayarishaji milioni 40 alafu aniletee dharau, hajui hiyo hela nimeipata vipi. Wengi wao wamekuwa na dharau kama vile wanafanya kazi bure, ndiyo maana nimekuwa nikifanya kazi nje ya nchi
alisema Diamond.
Akifafanua zaidi, alisema unaweza ukamweleza mtayarishaji mfike studio saa 12 asubuhi, lakini atakuja saa nne.
Kwangu hizo ni dharau, kama unaweza kuachana naye, yaani ukishamlipa hela ndiyo kabisa ni mapozi tu
alisisitiza.
Diamond, mmoja wa nyota mahiri wa muziki wa Bongo fleva nchini, kwa sasa anatamba na ngoma yake ya ‘Mdogo mdogo’ aliyoifanyia nchini Afrika Kusini chini ya mtayarishaji mahiri, Godfather.

0 comments:

Chapisha Maoni