Kiongozi wa kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese
jijini Dar es Salaam, Ahmad Ally ‘Madee’, amesema muziki wa sasa ni
mgumu kutokana na utitiri wa wasanii, hivyo kuwepo kwa kazi nyingi
mtaani.
Madee alisema jana kuwa kurundikana kwa nyimbo sokoni sio tu kunawapa
wakati mgumu wasanii, pia vituo vya redio na televisheni katika
kuchagua kazi za kuzitumia.
Yaani kwa wiki moja zinaweza zikatoka nyimbo nyingi, mpaka nyimbo yako ichezwe sio rahisi sana, hivyo wananchi wanashindwa kukuelewa kwa sasa wimbo hauchezwi redioni mara kwa mara
alisema.
Alisema kwa upande wake, imekuwa rahisi mashabiki kumpokea kwa haraka kutokana na kukaa muda mrefu katika soko hilo.
Madee ni msanii anayetamba na ngoma yake ya ‘Pombe Yangu’ inayofanya
vizuri katika muziki huo licha ya uwepo wa kazi nyingi katika soko.
0 comments:
Chapisha Maoni