Madereva wa pikipiki wamevamia kituo cha polisi cha kinone mvuha
wilaya ya Morogoro kwa kupiga mawe na kumjeruhi askari mmoja na kisha
kumtorosha mtuhumiwa aliekuwa anashikiliwa kwa makosa ya kubebe abiria
watatu katika pikipiki moja.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul akizungumza na
vyombo vya habari amesema madereva hao walikua wakishinikiza mwenzao
kuachiliwa huru ambapo kabla ya tukio madereva wa pikipiki walifanya
mgomo kisha kuandamana ambapo alivamia kituo cha polisi na kupiga mawe
na kumjeruhi askari mmoja na kufanikiwa kumtorosha mtuhumiwa ambapo
jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu 18 wanaosadikiwa kuhusika
na tukio hilo na watafikishwa mahakamani.
0 comments:
Chapisha Maoni