Jumatano, Agosti 06, 2014

BOKO HARAM WASABABISHA ONGEZEKO LA WAKIMBIZI NIGERIA

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa karibu watu 650,000 wameyakimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Idadi hiyo iliyotangazwa Jumanne hii na ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) inaashiria ongezeko la watu wapatao laki mbili tangu mwezi Mei mwaka huu. Ocha imeongeza kuwa watu 436,608 wamezihama nyumba zao huko katika majimbo ya Adamawa, Borno na Yobe ambako ilitangazwa sheria ya hali ya hatari mwezi Mei mwaka jana. Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa Wanaigeria wengine wasiopungua 1000 wamekimbilia katika kisiwa kimoja kilichopo katika ziwa Chad huko katika mpaka wa kaskazini mashariki wa Nigeria.

0 comments:

Chapisha Maoni