Tarehe 6 Agosti miaka 69 iliyopita Marekani, kwa mara ya kwanza iliushambulia kwa mabomu ya nyuklia na kuusambaratisha mji wa Hiroshima huko Japan mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia. Mabomu hayo yalikuwa na nguvu kubwa ya uharibifu ya mada za TNT zenye uzito wa tani elfu 20. Katika mashambulizi hayo watu zaidi ya elfu tisini waliuawa na wengine 75 elfu kujeruhiwa. Licha ya kupita miaka 69 sasa tangu Marekani ifanye mashambulizi hayo ya silaha za nyuklia katika mji wa Hiroshima huko Japan, lakini athari zake mbaya bado zinaendelea kushuhudiwa hadi hii leo.
Muda mfupi baada ya kuushambulia mji wa Hiroshima, Marekani iliushambulia pia kwa mabomu ya nyuklia mji wa Nagasaki huko huko Japan. Maafa hayo ya kutisha na kusikitisha yaliyofanywa na Marekani katika miji miwili ya Japan yanaonyesha hatari ya kumilikiwa silaha za nyuklia na nchi zinazopenda kujitanua duniani kama Marekani na ndiyo maana kuna udharura wa kusimamiwa na kudhibitiwa silaha hizo na taasisi husika na hatimaye kutokomezwa kabisa kwa ajili ya usalama wa dunia.
Siku kama ya leo miaka 133 iliyopita alizaliwa Alexander Fleming tabibu, mwanabiolojia na mtaalamu wa madawa wa Scottland. Tabibu huyo pamoja na wasomi wenzake wawili Chain na Florey waligundua mada ya dawa ya antibiotic yaani Penicillin wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Mwaka 1945, wasomi hao watatu kwa pamoja walitunukiwa tuzo ya Nobel katika taaluma ya tiba kutokana na ugunduzi wao huo muhimu. Penicillin inatumika sana katika elimu ya tiba.

0 comments:
Chapisha Maoni