Alhamisi, Agosti 07, 2014

LAMPARD AONESHA FURAHA YAKE YA KURUDI NYUMBANI

Kiungo kutoka nchini Uingereza Frank James Lampard ameanza mazoezi pamoja na wachezaji wa klabu ya Man City baada ya kusajiliwa kwa mkopo na mabingwa hao akitokea nchini Marekani kwenye klabu yake ya New York FC.
Lampard amerejea nyumbani ikiwa ni siku chache baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na New York FC kama mchezaji huru kufuatia mkataba wake na klabu ya Chelsea kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita.
Akizungumza kwa mara ya kwanza kupitia kituo cha televisheni cha Man city, Lampard amesema anajihisi furaha kurejea nyumbani na kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoitumikia klabu bingwa nchini Uingereza.
Amesema pamoja na kutarajia kuwepo klabuni hapo kwa kipindi cha miezi sita, bado anaamini mchango wake utaonekana kwa kiasi kikubwa na pengine kufikia sehemu ya mipangilio iliyowekwa hapo Etihad Stadium.

0 comments:

Chapisha Maoni