Alhamisi, Agosti 07, 2014

MAITI ZA WALIOKUFA KWA EBOLA ZATUPWA HOVYO MITAANI LIBERIA

Ugonjwa wa Ebola unaendelea kuwa tishio kubwa kwa watu Afrika Magharibi huku idadi kubwa ya watu ikipoteza maisha.
Kufuatia hofu ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari kwa kugusa au kuwa karibu na wagonjwa au miili ya waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo, ndugu wa marehemu wameripotiwa kuiburuza miili ya ndugu zao kutoka majumbani kwao na kuitupa hovyo mitaani hali inayoongeza hatari zaidi ya maambukizi.
Kwa mujibu wa Daily Mail, ugojwa huo hatari unaoweza kusababisha mtu kutokwa na damu machoni, mdomoni na masikioni umeshaua takribani watu 9,000 katika nchi za Afrika Mashariki.
Madaktari wanaohudumia wagonjwa wa Ebola wanapata changamoto kubwa ya kukwepa maambukizi huku baadhi yao wakiripotiwa kupata maambukizi na kupoteza maisha.
Hali ya hatari imesababisha abiria wanaosafiri kutoka Afrika Magharibi kufanyiwa vipimo katika viwanja vya ndege kwa hofu ya kuusambaza ugonjwa huo katika nchi wanazokwenda.

0 comments:

Chapisha Maoni