Kikongwe wa miaka 80 aliyetambulika kwa jina la adam mwandiga mkazi wa kijiji cha kibisi aliuawa kwa kupigwa fimbo kichwani na mohamed mwamela ambaye alikuwa anaishi naye [mtoto wa mdogo wa marehemu].
Tukio hilo limetokea tarehe 15.08.2014 majira ya saa 22:30 usiku huko katika kijiji cha Kibisi, kata ya Kyimo, tarafa ya ukukwe, wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya. Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia kati ya marehemu na mtuhumiwa.
Marehemu alikuwa akiishi na watoto wake wengine wawili ambao hawakuwepo wakati tukio hilo linatokea. Mtuhumiwa alikimbia mara baada ya tukio, juhudi za msako kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi mkoa wa Mbeya Barakael N. Masaki anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio hili azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. Aidha anatoa wito kwa wanafamilia kutatua migogoro yao ya kifamilia kwa njia ya amani na utulivu ili kuepuka madhara yanayoweza kuepukika.

0 comments:
Chapisha Maoni