Jiwe hili lipo katika kata ya ilima, nje kidogo ya mji wa Tukuyu katika
barabara ielekeayo Kyela, ni jiwe ambalo juu yake kuna chuma ambacho
hakijafungwa kwa nati wala kitu chochote lakini hakitikisiki wala
hakitoki, inasemekana jiwe hili liliwekwa enzi za ukoloni na koloni la
mwingereza. Miaka kadhaa iliyopita wananchi wa eneo hili walitaka kujua
chini ya jiwe kuna nini? ndipo walipoamua kuchimba ili kujua kuna nini
lakini hawakukuta kitu chochote.
Baada ya kukuta hakuna kitu chochote ndipo walipotaka kuliangusha ili
lisiwepo kabisa walijaribu kutaka kuliangusha pasipo mafanikio kwa
sababu halikuonesha mwisho wake ni wape kwa kwenda chini.
0 comments:
Chapisha Maoni